Tanganyika ina vivutio vingi sana kama vifuatavyo,
-Maporomoko ya Nkondwe
-Mto ambao ukinywa maji yake unapata watoto mapacha
-Sokwe wengi zaidi ya 1000 wanaopatikana katika misitu ya Tongwe Mashariki na Magharibi (Tanganyika)
-Mambo kale katika tarafa ya Karema
-Samaki anayetoa umeme
VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO WILAYA YA TANGANYIKA (MPANDA DC)- MKOANI KATAVI -
NA.
|
KIVUTIO CHA UTALII
|
MAHALI KILIPO
|
SIFA ZAKE
|
1
|
Hifadhi ya Taifa ya Katavi (Katavi National Park)
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
|
Hifadhi hii ni ya tatu kwa ukubwa baada ya hifadhi ya taifa ya Ruaha na Serengeti. Hifadhi ya Taifa ya Katavi inasifika kwa kuwa na:-
Makundi makubwa ya Viboko, Simba, Pundamilia na Nyati Uwepo wa mzimu wa kiume wa Wabende ujulikanao kama Katabi na mzimu wa kike wa Wamweru Uwepo wa Twiga mweupe Uwepo wa mabonde muhimu ya Ziwa Chada, Paradise na mbuga ya Katsunga Mazingira asilia yenye uoto wa misitu jamii ya miombo Uwepo wa Tembo wakubwa Maporomoko ya Mto Ndido na Chorangwa Uwepo wa aina mbalimbali za ndege |
2
|
Pori la Akiba la Rukwa (Rukwa Game Reserve)
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
|
Hifadhi hii inasifika kwa kuwa na:-
Makundi makubwa ya Viboko, Simba, Pundamilia na Nyati Uwepo wa Vitalu 3 vya Uwindaji wa Kitalii ambavyo ni Ziwa Rukwa, Mlele South na Rungwa river (Kimoja cha daraja la kwanza na 2 vya daraja la pili) Wanyamapori adimu kama Mbwamwitu, Puku (Sheshe) ambao ndiko sehemu pekee wanapatikana katika Pori hili na Kilombelo Maporomoko ya Mto Ndido na Yeye Uwepo wa Ziwa Rukwa Mazingira asilia yenye uoto wa misitu jamii ya miombo Uwepo wa safu za mlima wa Mulele Hills ambazo zinaweza kutumika kuweka Picnic sites Uwepo wa zaidi ya species 350 za ndege kama vile “Crown crane maarufu kama ndege chai” Uwepo wa mapango ambayo hutumika kwa ajili ya matambiko |
3
|
Ziwa Tanganyika
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (Kata ya Karema na Ikola)
|
Ziwa hili linasifika kwa:-
Ziwa la kwanza kwa Ukubwa katika Bara la Afrika na la pili Duniani (ukubwa 32,900 sq km) La pili kwa kuwa na umri mkubwa Duniani unaokadiriwa kuwa miaka 5500 La pili kwa kuwa na kina kirefu Duniani (kina 1,470 m) La kwanza kwa urefu kwa maziwa yenye maji laini (urefu ni 673 kms) Kuwa na zaidi ya ‘species’ 250 za samaki wa mapambo (Cichlid) ambao wanapatikana katika Ziwa hili pekee (endemic species) Uwepo wa fukwe nzuri za mchanga (sand beaches) Uwepo “Nile Crocodiles” Uwepo wa Samaki aina ya Nyika (electric fish) Uwepo wa meli kongwe ya MV Liemba iliyotengenezwa mwaka 1913. |
4
|
Ziwa Rukwa
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
|
Ziwa hili ni:-
Ni nne kwa ukubwa hapa nchini (5760 sq km) Lina idadi kubwa ya viboko, mamba na zaidi ya ‘species’ 350 za ndege tofauti tofauti Halitoi maji yake bali linapokea tu maji kutoka kwenye mito mikubwa mitano ambayo ni Kavuu, Rungwa, Yeye, Ilemba na Momba |
5
|
Chemichemi ya Majimoto
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
|
Hii ni chemichemi ambayo:-
Inatoa majimoto muda wote yenye nyuzi joto (0c) 40 Chimbuko la kabila la Wapimbwe |
6
|
Kanisa la Wapentekoste lililopo eneo la Katumba
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
|
Ni kanisa ambalo:-
Hili ni kanisa kubwa ambalo lina uwezo wa kubeba watu zaidi ya 700 Lilijengwa mwaka….. na mafundi wa mtaani Halina nguzo hata moja |
7
|
Kijiji cha kihistoria cha Karema
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
|
Eneo hili ni:-
Eneo la kihistoria mbalo historia yake inaanzia miaka ya 1885 tangu enzi wamisionari walipoingia Kuna mabaki ya historia ya mtakatifu Adrian Atman ambaye alikaa Karema kwa kipindi cha miaka 67 |
8
|
Misitu ya Hifadhi
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
|
Misitu hii ni:-
Eneo lake ni takribani asilimia 59 ya eneo lote la Mkoa Ina vivutio vingi vya utalii kama vile uwepo wa uoto wa asili aina ya miombo Sifa ya kuwa na Mapori tengefu (Game Controlled Areas) na hivyo kutumika kwa shughuli za uwindaji wa kitalii Uwepo wa miamba kama vile Magorofani, Safu za milima na mabonde |
9
|
Uwepo wa Sokwe Mtu
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
|
Mkoa wa Katavi unakadiriwa kuwa:-
Sokwe mtu zaidi ya 1000 ambao wanapatikana katika maeneo yaliyohifadhiwa (Msitu wa Hifadhi wa Tongwe Mashariki, Msitu wa Hifadhi inayopendekezwa ya Tongwe Magharibi na Msitu wa Mnimba ambao ni msitu wa hifadhi wa Kijiji cha Vikonge) Pia, Sokwe wanapatikana katika safu za milima ya Wansisi |
10
|
Maporomoko ya Maji
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
|
Mkoa una maporomoko ya:
Mto Nkondwe haya yanapatikana mita chache kutoka barabara ya Mpanda – Kigoma na yapo eneo zuri kwa ajili ya kuweka kambi za wageni Mto Mnyangwa ambayo yanapatikana katika Msitu wa hifadhi wa Tongwe Mashariki Luegele katika Mto Lwega Maporomoko ya Ntakata yanapatikana ndani ya Msitu wa Hifadhi tarajiwa ya Tongwe Magharibi Maporomoko ya Kilida katika Safu za Milima ya Lyamba lya Mfipa |
10
|
Historia ya Makabila ya Wabende, Wakonongo, Wapimbwe na Wafipa
|
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
|
Makabila haya yanasifika kwa:-
Kuwa na ngoma za jadi Matambiko ya kimila |
11
|
Safu za milima ya Lyamba lya Mfipa na Mulele
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
|
Safu hizi zinasifika kwa:-
Zinatoa mwonekano mzuri wa Ziwa Rukwa na mwonekanao mzuri wa uoto wa asili wa Miombo Mwonekano mzuri wa kuchomoza na kuzama kwa jua Milima ya Lyamba dio milima unapatikana pande zote za Ziwa Tanganyika Ni kati ya milima ambayo inatengeneza bonde la Ufa |
12
|
Chemichemi za Mito Sabagha na Kasewa na Wamweru
|
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
|
Sifa za chemichemi hizi ni:
Ni vyanzo vya maji ambayo maji yake yanatoka ardhini kwa presha (water fountain) Chemichemi ya Sabagha ndicho kinatoa maporomoko ya Nkondwe |
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.