• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

Hotuba za Viongozi Mbalimbali

MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU WATANZANIA WAPYA WALIOPEWA URAIA KATIKA MAKAZI YA KATUMBA, MISHAMO NA ULYANKULU.

 

Serikali imeweka wazi msimamo wake kuwa inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi na kusisitiza vitendo vya ubaguzi wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka kubaguana kisiasa,kidini na kwa namna yeyote hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe  Mwigulu  Lameki Nchemba wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba iliyoko katika  Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kujiepusha na vitendo vya kubaguana.

 Akizungumzia kuhusu Uzalendo wa kuipenda nchi asisitiza na kuwataka raia hao kuepukana na tabia ya za chuki dhhidi ya nchi yako badala yake uzalendo uwe mbele kwanza kwa nchi.

Mapema Mhe  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amesema kuhusu suala la maeneo ya makazi kufutwa hati ya kuwa makazi, amesema eneo hilo haliwezi kufutwa hati ya kuitwa makazi  hadi taratibu za kuhakikisha wale wote wanaoishi katika makazi hayo ni raia wa Tanzania na hakuna mkimbizi katika maeneo hayo lakini kama kutakuwa bado wapo wakimbizi hati haiwezi kubadilishwa hadi taratibu zikamilike.

Pia amewasisitisitiza kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.

Mapema Mkuu wa Makazi ya Mishamo na Katumba Athman Igwe alieleza kuwa kata ya Katumba ni ya muda mrefu na ilianzishwa mwaka 1972 hadi kufika sasa kuna wakazi zaidi ya 78,000 lakini asilimia tisini na saba ni ya raia wapya hivyo bado kuna wakimbizi kwenye eneo hili.

Hivi karibuni kulikuwa na zoezi la kuhakiki wakimbizi kwa ajili ya kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu zoezi lilianza tarehe 16 mwezi wa saba na limekamilika kwenye makazi haya mapya mwaka huu tarehe 3/8/ 2017 waliosajiliwa waliohakikiwa ni wakimbizi 11,329 kwa maana hiyo kuna kaya 5,134.

Pia Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewaasa watanzani wapya wanaoishi makazi ya Katumba na Mishamo Mkoani Katavi kuondoa fikra ya kuwa wao bado  ni wakimbizi badala yake wawe huru kwenda kuishi sehemu yeyote katika nchi maadamu wafuate taratibu na kuwasisitiza wale ambao hawajachukua vyeti vyao vya uraia wavichukue .

 Akihutubia kwenye mkutano wa Hadhara katika makazi ya Katumba na Mishamo Waziri Mwigulu ameeleza,na kuwasisitiza raia hao wapya na wale waliopatiwa vyeti vya uraia lakini hawataki kuchukua vyeti vyao waamue moja ama wachukue au waondoke kurudi kwao kwa kuwa kulikuwa hakuna haja ya kuomba uraia huo kama walikuwa hawautaki.

  Akizungumzia kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine katika nchi hii amesema ni jambo jema lakini amewaomba wasibadili majina yao bila kufuata utaratibu

Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga amewaasa kutunza mazingira pamoja na kusisitiza suala la kujitokeza kujiandisha kwa wale ambao hawakuandikishwa.

 Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Saidi Mselem amemweleza Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa wananchi wa Mishamo na Katumba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika maeneo hayo kwa kuwa wako watanzania wapya na wale walioandikishwa.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA May 27, 2025
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • HALMASHAURI ZA WILAYA YA MOMBA NA MAKETE ZAKUTANA WILAYANI TANGANYIKA KUJIFUNZA BIASHARA YA KABONI.

    May 26, 2025
  • TANGANYIKA KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA SUALA LA LISHE, WAKUU WA IDARA YA ELIMU NA WAKUU WA SHULE WAPEWA MBINU KUSIMAMIA UPATIKANAJI CHAKULA MASHULENI.

    May 13, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.