Seksheni hii lengo lake ni kutoa huduma za kitaalamu katika nyanja za Mipango, Bajeti na vilevile kuratibu shughuli za Halmashauri katika kutoa uwezeshaji wa utaalamu kwa Serikali za Vijiji. Seksheni hii inaongozwa na Mkuu wa Idara ya Mipango na Takwimu na Ufuatiliaji anayewajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji.
Idara hii ina shughulika na mambo yafuatayo:-
Kuratibu suala zima la maendeleo ya kiuchumi kwenye Wilaya ikijumuisha Sekta Binafsi, Mashirika, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za kijamii.
Kushauri na kuratibu utekelezaji wa sera za sekta mbalimbali katika Wilaya
Kuratibu maandalizi, usimamizi na tathimini ya mipango (Mpango Mkakati, Mpango Kazi na Bajeti) kwa ajili ya Sekretarieti ya wilaya.
Kuchambua, kuunganisha na Kusimamia maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Wilaya na Bajeti
Kuratibu miradi inayofadhiliwa na wafadhili/wadau wa maendeleo na kushauri shughuli za utekelezaji wa Miradi.
Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji kuhusu shughuli na majukumu ya mashirika, taasisi za kijamii na sekta binafsi
Kushauri na kuratibu shughuli za utafiti katika Wilaya
Kuratibu mazoezi ya sensa ya watu na makazi
Kuratibu shughuli zitokanazo na majanga katika wilaya
Kuzisaidia na kuzishauri Serikali za vijiji juu uibuaji wa Miradi.
Kuratibu utekelezaji na kusimamia ushiriki wa sekta binafsi katika masuala mbalimbali ya maendeleo
Kusimamia na kutathimini utendaji wa Mamlaka za Seriklai za Mitaa katika Mkoa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.