TAARIFA FUPI YA MRADI WA KUPASUA NA KUSAGA KOKOTO KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi huu wa kupasua na kusaga kokoto unamilikiwa na watu tisa waliojiunga katika kikundi kiitwacho YADAMO GROUP KABUNGU. Mradi huu ulianza mwaka 2012 ambapo utafiti wa eneo hili ulionyesha uwepo wa mawe ya kutosha kuanzisha kiwanda hiki. Mradi umeanza rasmi uzalishaji baada ya kusajiliwa mwaka 2016 kwa Reg. Na. BN 17022AA6FB46GB tarehe 24.10.2016 na unalipiwa kodi na tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi huu umegharimu jumla ya Tshs. 458,000,000.00 ambazo zimegharimiwa na wamiliki wa mradi. Hata hivyo wadau wa mradi huu wanategemea kukopa kwenye taasisi za kibenki kiasi cha shilingi 600,000,000.00 ili kununua mitambo kwa ajili ya kuongeza ufanisi na uzalishaji katika kiwanda hiki. Mpaka sasa kiwanda kimetoa ajira kwa watu 20 hususan vijana.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, katika eneo hili la mradi tunategemea kujenga uzio kuzunguka kiwanda hiki na pia kujenga nyumba na ofisi za wafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Matarajio ya mradi huu taasisi za umma, makampuni na wajenzi binafsi kutoka nje na ndani ya halmashauri ya wilaya ya Mpanda kununua kokoto zitakazozalishwa na kiwanda hiki.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, pamoja na ufanisi kiasi uliopatikana katika kiwanda hiki ambao kimsingi ni utekelezaji wa kauli mbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya ”Tanzania ya viwanda” changamoto kubwa inayotukabili sisi kama wadau wa maendeleo katika kiwanda hiki ni kukosekana kwa umeme na kulazimika kutumia jenereta ambayo inaongeza gharama kubwa katika uzalishaji.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, kwa heshima na taadhima tunaomba utuwekee jiwe la msingi katika kiwanda hiki ambacho kinatarajiwa kuingizia halmashauri ya wilaya ya Mpanda mapato na kutoa fursa zaidi za ajira hasa kwa vijana wa Wilaya ya Tanganyika.
Naomba kuwasilisha,
Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeeee!!!
TAARIFA YA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA ITETEMYA KATA YA KAREMA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mradi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Itetemya tarafa ya Karema unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali kuu kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF III kwa kushirikianana wananchi pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
GHARAMA ZA MRADI
Mchango wa serikali kuu ni…………………………….Tshs. 66,000,000.00
Mchango wa jamii ni…………………………………….. Tshs.6,891,800.00
Mchango wa halmashauri…………………………….… Tshs. 3,500,000.00
JUMLA KUU 76,391,800.00
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, lengo la mradi huu ni kutekeleza miradi katika maeneo yenye upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya na elimu kwa walengwa (kaya masikini) kutokana na tathmini ya uwezo wa vituo vya kutolea huduma za afya na elimu iliyofanyika wa kati wazoezi la uandikishaji wa walengwa.
Ndugu Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Manufaa ya mradi huu nikupunguza msongamano wahuduma katika kituo cha afya Karema kwa wananchi wa kijiji cha Karema na vijiji vya jirani nakuwawezesha walengwa kutimiza masharti ya afya kwaurahisi zaidi hivyo kuendelea kupata ruzuku kutoka TASAF III ili kutimiza dhana ya mpango ya kunusuru kaya masikini.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, kwa heshima na taadhima tunakuomba sasa uweke jiwe la msingi katika mradi huu wa zahanati ya kijiji cha Itetemya ambao ukikamilika unatarajiwa kutoa huduma kwa kaya zipatazo 501 pamoja na vijijiji vya jirani.
Naomba kuwasilisha
Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeee!!!!!!!!!
TAARIFA FUPI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGEWA UHURU KITAIFA NDUGU AMOUR HAMAD AMOUR
Ndugu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, mikopo ya wanawake na vijana ni miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ili kuwapunguzia wanawake na vijana ugumu wa maisha na kuongeza ajira.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, katika kipindi cha Julai 2016 hadi Aprili 2017 Halmashauri imetoa mikopo yenye jumla ya shilingi 86,650,000 kwa vikundi vya Wanawake na Vijana. Mchango wa asilimia 5 kwa vijana na asilimia 5 kwa wanawake kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri.
Hadi tarehe 2/4/2017 jumla ya shilingi 56,750,000 zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana na wanawake kama ifuatavyo;
Ndugu Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, kwa heshima na taadhima tunakuomba leo tarehe 3/4/2017 ukabidhi hundi 9 zenye thamani ya Tshs. 12,300,000 kwa vikundi 9, ambapo kati ya vikundi hivyo, vikundi 3 ni vya vijana vinavyopokea jumla ya Tshs. 3,700,000 na vikundi 6 vya wanawake vinapokea jumla ya Tshs 8,600,000. Aidha vikundi 4 vya vijana vinapokea pikipiki 8 zenye thamani ya Tshs 17,600,000. Mikopo ina jumla ya Tshs. 29,900,000 ambayo itawanufaisha wanavikundi na itarejeshwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa riba nafuu ya asilimia 10.
Naomba kuwasilisha,
Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeeee!!!!!!!!!!!
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.