Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendesha doria katika misitu ya hifadhi ya biashara ya Kaboni, kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama ya Wilaya imefanikiwa kubaini ekari 9 zilizolimwa madawa ya kulevya aina ya Bangi na kuziteketeza kwa moto katika msitu wa kijiji cha Kapanga.

Hatua hiyo imejiri ikiwa ni juhudi madhubuti za kuilinda misitu hiyo, isiendelee kuharibiwa na baadhi ya watu wanaovamia na kujihusisha na shughuli za kibinadamu kinyume na utaratibu.
Katika zoezi hilo la uchomaji wa mashamba hayo lililoongozwa na Mamlaka ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya kanda ya Tabora, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu amekemea vikali tabia za kuendesha shughuli za kilimo pamoja na kilimo cha bangi katika maeneo ya misitu ya vijiji haswa ya biashara ya kaboni, akiwaelekeza kuacha mara moja na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika au kukamatwa akifanya shughuli hizo.

Sambamba na hilo amewataka wananchi wanaovamia maeneo ya misitu ya biashra ya kaboni, kuacha kulima bangi na kujihusisha zaidi ya kilimo cha mazao mengine yenye fursa za kiuchumia kama pamba, tumbaku na ufuta tena katika maeneo yaliyorasimishwa kwaajili ya shughuli hizo.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Rasilimali watu na Utawala Bw Clavery Reginald amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika itaendelea kuratibu zoezi la doria mbalimbali kwa maeneo yote ya misitu iliyotengwa kwaajili ya biashara ya kaboni na maeneo yote ya uwekezaji ili kuilinda isiharibiwe na watu wenye nia ovu.

Biashata ya Kaboni katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imenufaisha vijiji 8 ambapo kwa kijiji cha Kapanga pekee wastani wa Tsh Bilioni moja 1,000,000,000/= zimeingizwa katika kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya mapato yatokanayo na biashara hiyo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.