Halmshauri ya wilaya ya Mpanda ilianzishwa 1983 na ilikuwa ndani ya mkoa wa Rukwa. Mwaka 2012 wilaya ya Mpanda iligawanywa na kuzaa wilaya ya Mlele na Mpanda yenyewe. Mkoa wa Katavi umeanzishwa 2012 baada ya kuigawanya halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kupata wilaya 3 na halmashauri za wilaya 5. Wilaya hizo ni wilaya ya mpanda ambayo ina halmashauri za wilaya 2 ambazo ni halmashauri ya Manispaa ya mpanda na halmashauri ya wilaya ya Nsimbo.
Wilaya ya Mlele ina halmashauri 2 ambazo ni halmashauri ya wilaya ya Mlele na halmashauri yawilaya ya Mpimbwe. Wilaya ya Tanganyika ina halmashauri 1 ambayo ni halmashauri ya wilaya ya Mpanda (halmashauri mama).
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ilianzishwa rasmi mwaka 2016 na ina Tarafa 3 ambazo ni Mwese, Kabungu na Karema, pia ina kata 16 na Vijiji 55 ambavyo vinauda jimbo moja la Mpanda Vijijini.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.