MUHTASARI WA KIKAO CHA KAMATI YA UKIMWI KILICHOFANYIKA TAREHE 02/01/2018 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA MAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
WAJUMBE WALIOHUDHURIA
WAJUMBE (WAALIKWA)
WATAALAM WALIOHUDHURIA
SEKRETARIETI
AGENDA NA. HW/MPN/01/01/2018: KUFUNGUA KIKAO.
Katibu alianza kwa kuwasalimu wajumbe na kuwakaribisha kwenye kikao na kuwatakia wajumbe heri ya mwaka mpya.Alimkaribisha Mwenyekiti afungue kikao. Mwenyekiti aliwasalimu wajumbe kwa kuzingatia itifaki na kuwatakia heri ya mwaka mpya. Aliwata radhi wajumbe kwa kikao kuchelewa kuanza huku akisema kuwa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo.Alifungua kikao saa 5:34 asubuhi.
AGENDA NA. HW/MPN/02/01/2018: KUTHIBITISHA AGENDA
Agenda saba (07) zilisomwa kwenye kikao na ziliafikiwa. Agenda hizo zilikuwa Kama ifuatavyo:-
AGENDA NA. HW/MPN/03/01/2018: KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO CHA TAREHE 02/10/2017.
Muhtasari wa kikao kilichopita ulisomwa,ukaridhiwa kwa ajili ya kumbukumbu za Halmashauri.
AGENDA NA. HW/MPN/04/01/2018: KUSOMA YATOKANAYO
Utekelezaji wa maagizo ya kikao cha tarehe 02/10/2017 ulisomwa kama ifuatavyo:-
SUALA LA MIRADI YA ILANDAMILUMBA SEKONDARI
Ilikuwa imeagizwa kuwa shule ya Ilandamilumba itembelewe kuona miradi yake iliyopo( mradi wa kuku na mbuzi)
UTEKELEZAJI
Ilielezwa kuwa baada ya kutembelea shule hii, timu ilikuta mapungufu katika usimamizi wa klabu na miradi hii haipo. Kutokana na klabu kutosimamiwa vizuri miradi mingi ilikufa.Hata hivyo mwalimu mkuu ameahidi kuboresha klabu hii kwa kuteua mwalimu mlezi mwingine na kusaidia pale inapohitajika.Kitengo cha UKIMWI na idara ya elimu sekondari wataendelea kufuatilia klabu hii na kuirejesha katika uhai wake.Utekelezaji umeafikiwa
SUALA LA WATUMISHI WANAOISHI NA VVU
Ilikuwa imeagizwa kuwa watumishi wanaoishi na VVU huko katani washawishiwe wajitokeze ili kupata takwimu zao halisi.
UTEKELEZAJI
Ilielezwa kuwa watumishi wanaoishi na VVU/UKIMWI katani ushawishiwa kupitia vikao vya idara zao au mikutano jumuishi.Hata hivyo, suala la kujitokeza ni utashi na maamuzi ya mtu binafsi pasipo kumlazimisha au namna yoyote ya kutumia nguvu.Halmashauri kupitia kitengo cha UKIMWI kwa kushirikiana na idara na vitengo vingine inaendelea kuwasihi watumishi waishio na VVU/UKIMWI kujitokeza ili kupata takwimu sahihi na msaada pale inapohitajika. Utekelezaji haukuafikiwa. Iliagizwa kuwa utekelezaji wa agizo hili uwasilishwe kikao kijacho.Kadhalika,afisa utumishi ashirikishwe kwenye suala hili.
SUALA LA UPIMAJI UNAOFANYIKA KINYEMELA
Ilikuwa imeagizwa kuwa upimaji wa VVU unaofanyika kinyemela kwenye maduka ya dawa Kasekese ufuatiliwe ili kuthibitisha zoezi hili.
UTEKELEZAJI
Ilielezwa kuwa Idara imeandaa utaratibu wa kushitukiza wakati wowote. Utekelezaji uliafikiwa.
SUALA LA MIRADI YA MASHINE KAREMA
Ilikuwa imeagizwa kuwa mradi wa mashine ya kukoboa na kusaga iliyotolewa kwa WAVIU wa Karema ifuatiliwe kujua mustakabali wake.
UTEKELEZAJI
Ilielezwa kuwa baada ya kutembelea mradi, timu ilijiridhisha kuwa mradi upo kwa kuuona, isipokuwa kinu cha kusaga nafaka ni kibovu kutokana na bati zake kuharibika; pia nyumba ya mashine inahitaji kuimarishwa. Hata hivyo, wajumbe ngazi ya kata na tarafa wameomba mradi huu uamishiwe ngazi ya Kata kutoka tarafa ili kurahisisha usimamizi mzuri kutokana na baadhi ya wajumbe kutoka kata za mbali hivyo kushindwa kusimamia mradi vizuri na baadhi ya WAVIU wamekwisha kufariki dunia hivyo kuwa na uongozi mpya. Maelezo ya ufafanuzi zaidi yamo katika taarifa hii na muhtasari wa kuomba kuhamishwa mashine umekwisha wasilishwa. Utekelezaji uliafikiwa.
AJENDA NA. HW/MPN/05/01/2018: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI OKTOBA – DESEMBA ,2017
Taarifa iliwasilishwa kwenye kikao ambayo ilieleza shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Oktoba - Desemba, 2017 ikiwa ni pamoja na upimaji wa VVU kwa hiari,huduma ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Taarifa ya Mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi tarafa ya Karema ikiwa na pamoja na changamoto zinazoukabili mradi huo na mapendekezo ya wajumbe, Taarifa ya msaada wa fedha kwa watumishi wanaoishi na virusi vya ukimwi,Utoaji wa vyeti vya uthamini kwa wahitimu wa klabu za ukimwi,ufuatiliaji wa taarifa za klabu kwa shule za sekondari na changamoto zinazozikabili klabu hizo pamoja na utatuzi wa changamoto husika. Kadhalika, taarifa hii ilihusu pia taarifa kutoka kwa waelimisha rika kutoka kata mbalimbali,taarifa kutoka asasi za kiraia,taarifa za utekelezaji kutoka asasi ya KDF, taarifa ya kazi zilizofanywa na dawati la jinsia na watoto katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kutoka jeshi la polisi,changamoto mbalimbali zinazokikabili kitengo hiki ziliwasilishwa pia ikiwa ni pamoja na utatuzi wa changamoto hizo. Taarifa ilijadiliwa na kupokelewa na kushauriwa na kuagizwa yafuatayo
AGIZO
Takwimu za WAVIU wanaotumia dawa kwa kila kata zipatikane ili kujua hali ya maambukizi katika maeneo yetu hasa kata.
AGIZO
Gharama za kinu cha mashine ya kukoboa Karema ijulikane. Kadhalika,kikao kijacho itolewe taarifa kama mashine hiyo imeanza kufanya kazi au la.
AJENDA NA. HW/MPN/06/01/2017:MENGINEYO.
Hakukuwa na mengineyo. Kadhalika,katika kuhitimisha ajenda hii,yafuatayo yalielezwa:
MWENYEKITI WA HALMASHAURI
AJENDA NA. HW/MPN/07/01/2018: KUFUNGA KIKAO.
Katibu aliwashukuru wajumbe kwa kuchangia ajenda kwa umakini. Alimkaribisha Mwenyekiti afunge kikao. Kabla ya Mwenyekiti kufunga kikao, Aliishukuru meza kuu kwa mawazo mazuri. Kadhalika, aliwashukuru wajumbe, wawakilishi na wataalam kwa uchangiaji wao mzuri wa ajenda zilizowasilishwa. Alifunga kikao saa 7:30 mchana.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.