• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

Maendeleo ya Jamii

1.0 Utangulizi

Idara ya Maendeleo Jamii, na Ustawi wa Jamii ni miongoni mwa Idara 13 na vitengo 6 vinavyojitegemea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, na ni kiungo muhimu kati ya Halmashauri na jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za Halmashauri.

1.1 Muundo wa Idara

Idara ina vitengo Vikuu Vitatu ambavyo ni:

  • Maendeleo ya Jamii kikiwa na watumishi
  • Ustawi wa Jamii kikiwa na watumishi na
  • Maendeleo ya Vijana

1.2 Shughuli za Idara. 

1.2.1 Maendeleo ya Jamii

Kushirikisha jamii katika kubaini, kubuni, kupanga, kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango/miradi ya Maendeleo.

Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na watumishi wa sekta nyingine.

Kuelimisha viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali na viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Kuelimisha na kuhamasisha jamii kupambana na VVU na UKIMWI.

Kueneza elimu ya Uraia mwema.

Kufanya uchambuzi wa matatizo ya jamii na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi zingine.

Kuvisaidia vikundi maalum (vya ushirika, vikundi vya kijamii, vya kidini, n.k.) kuandaa miradi na kuwaelekeza namna ya kupata mitaji.

Kuelimisha jamii juu ya kutekeleza masuala ya kijinsia na kuratibu shughuli zote za Maendeleo ya Jamii kwa kuzingatia jinsia.

Kuhamasisha jamii kuondokana na mila/desturi zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda kuleta mabadiliko.

Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya wanawake.

Kuhamasisha jamii kutumia teknolojia rahisi na sahihi na.

Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya watoto.

Kuratibu maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

 

1.2.2 Ustawi wa Jamii

Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Miongozo, Kanuni na viwango vya ubora katika utoaji wa huduma mbalimbali za ustawi wa jamii.

Kufanya tathmini, ufuatiliaji na utaratibu wa huduma za ustawi wa jamii.

Kujenga uwezo wa kitaaluma kwa Maafisa Ustawi wa jamii ili waweze kutoa huduma timilifu kwa wananchi.

Kufanya tafiti zinazohusu huduma za ustawi wa jamii.

Kuwajengea uwezo watumishi wa ustawi wa jamii na Wadau katika utoaji wa huduma.

Kuanzisha na kuendeleza programu za kushawishi, kutetea na kulinda haki za makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu wa viungo na ngozi, wazee na wasiojiweza, familia zenye dhiki na watoto waishio katika mazingira hatarishi.

Kujenga Uhusiano na wadau wa nje na ndani ili kutoa huduma bora za ustawi wa jamii.

Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.

1.2.3 Maendeleo ya Vijana

  • Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana.
  • Kuratibu shughuli za mifuko/mikopo ya vijana.
  • Kuhamasisha vijana kufufua moyo wa kujitolea kwa ajili ya Maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
  • Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya uzazi na kujamiina kwa Vijana.
  • Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, ajira kwa vijana na elimu ya familia kwa kushirikiana na Vyama visivyo vya kiserikali.
  • Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu vijana.
  • Kuratibu shughuli za NGOs mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Vijana.
  • Kuandaa mpango wa kuboresha malezi ya vijana.
  • Kuhamasisha waajiri na wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa vijana katika maeneo mbalimbali.
  • Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo vijana ili kuwawezesha kujiajiri.
  • Kuandaa mipango ya kuhamasisha vijana ili kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiajiri.
  • Kuratibu shughuli za mabaraza ya vijana.
  • Kuandaa na kuratibu shughuli za matamasha ya vijana.
  • Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs na CBOs zinazofanywa ngazi ya Wilaya.
  • Kuratibu mafunzo ya utoaji wa mbinu za kuwasaidia vijana kujikomboa na umaskini, ujinga, kupiga vita UKIMWI, madawa ya kulevya na kutetea usawa wa jinsia.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • TANGANYIKA YAWEKA MIKAKATI KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO

    February 01, 2023
  • DC JAMILA AHIMIZA UPANDAJI NA UTANZAJI WA MITI

    January 24, 2023
  • Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Tanganyika yawataka watumishi kusimamia Ilani

    January 23, 2023
  • Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Tanganyika yawataka watumishi kusimamia Ilani

    January 23, 2023
  • Tazama zote

video

DC wa Tanganyika asisitiza michezo katika kata ya Bulamata
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.