https://matokeo.necta.go.tz/csee/csee.htm
MWAMTUKA kuinua elimu Tanganyika
Walimu wakuu, wakuu wa shule na maafisa elimu kata wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wamepewa mafunzo ya uwezeshaji wa uboreshaji wa matumizi ya mfumo wa wazi wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi (MWAMTUKA). Mafunzo hayo yamefanyika Desemba 8, 2018 katika ukumbi wa chuo Kikuu huria cha Tanzania, tawi la Katavi.
Akifungua mafunzo hayo, mgeni rasmi ambaye pia ni afisa utumishi katika ofisi ya katibu tawala wa mkoa Katavi Bw. Boko Majinge amewashauri walimu kujifunza kwa bidii namna ya kujaza mfumo huo wa upimaji wa utendaji kazi kwa waajiriwa (OPRAS) ili uinue elimu ya Tanganyika. Katika mfumo huo kuna vipengele muhimu 8. Kila kipengele kinaweza kusaidia kuinua elimu kama kitazingatiwa na kinaweza kushusha elimu kama kitapuziwa.
Ujazaji OPRAS ni mfumo wa wazi ambao unamtaka mwajiri na mwajiriwa au Mkuu wa Idara au kitengo akae na kila mtumishi aliyopo chini yake ili wajadili na kukubaliana malengo ya utendaji kazi kwa kipindi cha muda wa miezi 6 na baadaye kukaa tena pamoja kufanya tathmini ya nusu mwaka.
“Nawapongeza maafisa elimu wa Tanganyika kwa kuitisha mafunzo haya kwa viongozi hawa. Wengi wenu mlikuwa hamjazi OPRAS ama kwa kujua au kutokujua umuhimu wake. Ndiyo maana wengine walikuwa wanajaziwa na wengine kazi yao ilikuwa kuigilizia kwa mtu mwingine. Kila mmoja wenu akawajibike kuhakikisha anakaa na wa chini yake na kuweka makubaliano ya kiutendaji” Amesema Majinge
Naye afisa elimu msingi, Bw. Keny Shilumba amewaagiza walimu hao kuhakikisha kila mmoja anatumia mafunzo hayo vizuri ili wanafunzi wapate haki yao. Sifa ya mwalimu ni kufaulisha wanafunzi kwa njia zinazokubalika.
Hata hivyo, afisa elimu sekondari Bw. Michael Lyambilo amewaambia walimu kuwa siku hizi ni ukweli na uwazi, hivyo tusimamie miongozo na walaka na kanuni zinazoongoza masuala ya elimu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.