Disemba 5, 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeendesha mafunzo maalum ya ujazaji wa Rejesta za Wakazi kwa Watendaji wa Kata na Vijiji.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo juu ya namna sahihi na yenye ufanisi ya kukusanya na kuhifadhi taarifa za wakazi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.



Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuhakikisha taarifa za wananchi zinakuwa sahihi, za kuaminika na zenye kuleta tija kwenye mipango ya maendeleo.



Rejesta hio inafaida mbalimbali katika maendeleo ya jamii ikiwa ni Pamoja na:
• Kuhifadhi taarifa muhimu za kaya na wakazi
Husaidia kufahamu idadi ya watu, kaya, watoto, wazee na makundi mengine muhimu.
• Msingi wa mipango ya maendeleo
Takwimu sahihi hutumika kwenye kupanga na kutekeleza miradi ya afya, elimu, maji na huduma nyingine muhimu.
• Msingi wa mipango ya maendeleo
Takwimu sahihi hutumika kwenye kupanga na kutekeleza miradi ya afya, elimu, maji na huduma nyingine muhimu.
• Kusaidia misaada ya kijamii
Rejesta hutambua watu wenye uhitaji maalum kama wazee, yatima na watu wenye ulemavu.



TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.