• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

Makala Mbalimbali

SERIKALI HAITAMWONEA AIBU ASIYELIPA  

 KODI  YA MADINI 

 Kibada Ernest Kibada - Katavi.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini haitamwonea aibu mchimbaji yeyote wa madini atakayekwepa kulipa kodi Serikalini  kwa kuwa ni kinyume na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.Ameyasema hayo leo tarehe  Oktoba 11, 2018 katika  mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli zao katika machimbo ya  Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake  katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,  Salehe Mhando,  Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.Alisema kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wasio waaminifu wanaokwepa kulipa kodi serikalini hali inayokwamisha  upatikanaji wa huduma nyingine muhimu katika jamii kama vile elimu, maji, barabara.“ Mchimbaji ambaye anakwepa kulipa kodi mbalimbali kama Sheria ya Madini na kanuni zake inavyofafanua ni adui namba moja katika ukuaji wa maendeleo ya nchi, hivyo sisi kama Wizara ya Madini tumejipanga kuchukua hatua za kisheria nia ikiwa ni kutaka kila mwananchi anufaike na rasilimali za madini kupitia uboreshaji wa huduma mbalimbali,”alisema NyongoKatika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka maafisa madini wakazi katika mikoa yote kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa maduhuli kwani Sekta ya Madini inatarajiwa mno kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaamini kuwa iwapo Sekta ya Madini itasimamiwa kikamilifu, inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye  ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia uimarishaji wa sekta nyingine muhimu.Aidha, aliwataka maafisa madini nchini kushirikiana na  vyombo vya ulinzi na usalama katika wilaya kwenye zoezi la ukaguzi wa shughuli za madini ili kuongeza tija kwenye  ukaguzi.Katika mkutano huo mbali na wachimbaji wadogo kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya ya kusikiliza na kutatua changamoto kwenye  shughuli za uchimbaji madini katika mkoa wa Katavi, wachimbaji hao waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mahitaji ya mikopo katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, mafunzo kuhusu sheria ya madini na kanuni zake, uchimbaji salama na vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji wa madini.Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo katika eneo hilo, Imso Masumbuko kutoka kikundi cha Kagera Group alisema kuwa wana uhitaji mkubwa wa elimu kuhusu uchimbaji wa madini  salama pamoja na vifaa vya kisasa ili waweze kuzalisha na kulipa kodi zaidi Serikalini.Masumbuko mbali na kuainisha changamoto hizo aliiomba Wizara ya Madini kuiomba Wizara ya Nishati ili iweze kufikisha umeme katika machimbo hayo  kupitia Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu   REA IIIAlifafanua kuwa, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme katika eneo lao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye uzalishaji wa madini kutokana na matumizi ya dizeli hivyo kupata faida kidogo sana.Naye Karusum Daudi ambaye ni mchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini iangalie uwezekano wa kuwapatia mikopo ili waweze kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa.Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi na kusikiliza kero mbalimbali za watumishi ikiwa ni pamoja na kuzitatua.Pia Naibu Waziri Nyongo alikutana na wachimbaji wadogo wa madini mjini Mpanda lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini.Mbali na kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizotatuliwa na Naibu Waziri Nyongo papo hapo  wachimbaji wadogo wa madini walimpongeza Naibu Waziri Nyongo na kumwomba kuendelea na ari ya kusikiliza kero zao na kuzitatua.Akizungumza katika kikao hicho, Nyongo alisema Wizara ya Madini haitachoka kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini kwa kuwa inataka wachimbe katika mazingira mazuri na kulipa kodi Serikalini.  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya  Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake  katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe  Oktoba 11, 2018  

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini kutoka machimbo ya  Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani   kwenye mkutano wa hadhara

   


Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya  Dirifu, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi akiwasilisha kero yake mbele ya  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo. (hayupo pichani)

   

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akioneshwa mchoro wa ramani ya jengo linalojengwa la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi na  Mhandisi Andrew Mpangalala kutoka SUMA JKT ( wa kwanza kulia) ambao ndio wajenzi wa jengo hilo katika eneo la Msasani mjini Mpanda mkoani Katavi.


 

Naibu Waziri wa  Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kufanya nao kikao kilicholenga kujadili utendaji kazi.

 

(Picha zote na Kibada Ernest Kibada wa Katavi Press Club.)

 

MWISHO.

 


Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • TANGANYIKA YAWEKA MIKAKATI KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO

    February 01, 2023
  • DC JAMILA AHIMIZA UPANDAJI NA UTANZAJI WA MITI

    January 24, 2023
  • Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Tanganyika yawataka watumishi kusimamia Ilani

    January 23, 2023
  • Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Tanganyika yawataka watumishi kusimamia Ilani

    January 23, 2023
  • Tazama zote

video

DC wa Tanganyika asisitiza michezo katika kata ya Bulamata
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.