• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI TANGANYIKA

Posted on: January 19th, 2026

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imefanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 17 hadi 18 Januari, 2026 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026.Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi, kutathmini matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali pamoja na kubaini changamoto zinazoweza kuathiri ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati uliopangwa.

Katika ziara hiyo, Kamati imekagua ujenzi wa Shule ya Msingi Sibwesa unaojumuisha madarasa sita ya elimu ya msingi, madarasa mawili ya elimu ya awali, jengo moja la utawala pamoja na matundu kumi na manne ya vyoo kwa wavulana na wasichana. Kamati pia ilikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Itunya ambao kwa sasa umefikia hatua ya uwekaji wa dari na upigaji wa ripu.
Vilevile, Kamati imekagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Mchangani (Ikola), ambapo mradi huo upo katika hatua ya ufungaji wa renti huku mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi.Aidha, Kamati ilitembelea kikundi cha TUJIKOMBOE IKOLA GROUP chenye wanachama watano ambacho kimepokea mkopo wa shilingi 53,000,000 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa ajili ya ujenzi wa ghala (godown) na biashara ya ununuzi na uhifadhi wa mazao, ambapo Kamati ilipongeza juhudi za kikundi hicho katika kuimarisha uchumi wa wananchi.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya walimu aina ya 2:1 katika Shule ya Sekondari Juma Zuberi Homera, ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mchakamchaka, ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ifukutwa pamoja na ukaguzi wa utengenezaji wa madawati katika Kijiji cha Majalila.Baada ya kukamilisha ziara hiyo, Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ilieleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, ikibainisha kuwa miradi mingi inaendelea vizuri na inaonesha thamani ya fedha inayotumika. Hata hivyo, Kamati ilitoa maelekezo na ushauri mbalimbali ikiwemo kuhakikisha mafundi wanalipwa mara moja baada ya kukamilisha kazi walizokabidhiwa bila kucheleweshwa.Kamati pia ilielekeza vikundi vilivyopata mikopo kutoka Halmashauri kufuatiliwa kwa karibu na kuangaliwa namna ya kuviwezesha kupata mtaji wa kununua mazao ili kuimarisha na kuendeleza biashara zao.
Aidha, Kamati ilisisitiza ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mchakamchaka upewe kipaumbele kwa kuongezewa fedha ili ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Halmashauri ilishauriwa kutenga fedha mahsusi kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha ubora wa kazi na thamani ya fedha inayotumika.Vilevile, Kamati ilitoa maelekezo kwa mafundi na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi kuendelea kupewa elimu juu ya taratibu za uombaji wa zabuni na tenda kupitia mifumo rasmi ya Serikali ikiwemo Mfumo wa NeST, kabla ya kupewa kazi, ili kuongeza uwazi, ushiriki wa wazawa na ufanisi katika utekelezaji wa miradi.Kwa ujumla, ziara hiyo imeendelea kuonesha dhamira ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika katika kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo, kuhakikisha utekelezaji wake unazingatia mipango na bajeti, na kwamba wananchi wananufaika na huduma bora, endelevu na zenye tija kwa maendeleo ya jamii.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA May 27, 2025
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI TANGANYIKA

    January 19, 2026
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI TANGANYIKA

    January 19, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA DISEMBA 5,2025 IMEENDESHA MAFUNZO YA UJAZAJI WA REJESTA ZA WAKAZI.

    December 05, 2025
  • EKARI 9 ZA BANGI ZATEKETEZWA, MKURUGENZI NA DC TANGANYIKA WATOA MAAGIZO

    December 03, 2025
  • Tazama zote

video

DC BUSWELU ATAKA UWAJIBIKAJI WANUFAIKA WA MIKOPO TANGANYIKA DC
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.