Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika wa kwanza kuanzisha Wilaya hii na sasa Mbunge wa Jimbo la Kilindi mkoani Tanga, Salehe Mbwana Mhando, amepongeza utendaji na maendeleo ya Halmashauri ya Tanganyika, akiahidi kuijenga Kilindi kwa mfano wa mafanikio ya Tanganyika.
Akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tanganyika, Bw Shaban J. Juma, alipofika kusalimia, Mhando amesema kila anapofika Tanganyika hukutana na maendeleo mapya, jambo linaloifanya Halmashauri hiyo kuwa shamba darasa kwa Kilindi.
“Nikuhakikishie Mkurugenzi, nataka kuijenga Kilindi kwa mfano wa Tanganyika, ingawa tuna kazi kubwa ya kufanya kule… Kwa kuwa ninyi ni shamba darasa, nitashirikiana na Mkurugenzi wangu kule ili yanayotokea hapa yafanyike na kule,” alisema Mhando.

Kauli hiyo aliitoa Novemba 26, 2025, alipotembelea Ofisi za Wilaya ya Tanganyika, ambapo amepata fursa ya kuzungumza na watumishi na watendaji wa Halmashauri hiyo.
Sambamba na hayo, Mhe Mhando amewataka wananchi wa Tanganyika na Tanzania kwa ujumla kudumisha amani na utulivu, ili serikali iendelea kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wote.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.