Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Bw. Shabani J. Juma, amefanya kikao kazi na watendaji wa vijiji na kata, walimu wakuu, wakuu wa shule na wasimamizi wa miradi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Halmashauri, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kukamilishwa kwa wakati kama ilivyoainishwa kwenye mipango ya Halmashauri pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Mrindoko kutaka miradi yote ikamilike ifikapo Desemba 30.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mnamo Novemba 26, 2025, ambapo DED Shabani amesisitiza umuhimu wa ushirikiano mzuri kati ya watendaji wa kata na walimu wakuu ili kurahisisha utekelezaji wa miradi ya shule na kuhakikisha kazi zinakwenda kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi amewataka wahandisi na wasimamizi wa miradi kuongeza ufuatiliaji wa karibu na kufanya tathmini ya mara kwa mara ili kubaini changamoto zinazoathiri kasi ya utekelezaji wa miradi na kuzitatua mapema kabla hazijachelewesha malengo yaliyopangwa.
Ili kuongeza ufanisi, DED Shabani amesema Halmashauri itaunda timu ya wataalam kutoka idara na vitengo husika kwenda moja kwa moja kwenye maeneo ya miradi na kuweka kambi kwa muda, kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa papo hapo bila ulazima wa wahusika kusafiri hadi wilayani kufuata huduma.

Kikao hiki kimefanyika kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, aliyetoa maagizo kwa wilaya zote kuhakikisha zinakamilisha miradi yao yote ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.