Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu ameelezea kuridhishwa kwake na maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika eneo la Kamsenga,
Mheshimiwa Buswelu ameyasema hayo jana alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Mwezi wa Nne mwaka huu,
"Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu, lakini niwaombe Mkurugenzi na Mafundi mliosaini mikataba ya kujenga sekondari hii, kamilisheni mradi huu kwa wakati ili wanafunzi wetu waanze kusoma hapa mwezi wa nne" amesema DC Buswelu,
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Philemon Mwita amesema kuwa Ofisi ya Mkurugenzi itahakikisha shule hiyo inakamilika kwa wakati ili wanafunzi waanze kuyatumia madarasa hayo ifikapo mwezi wa nne mwaka huu,
Shule ya sekondari ya Kamsenga ni miongoni mwa miradi mingi ya elimu inayotekelezwa wilayani Tanganyika wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 600 ambao unatakelezwa katika eneo la Kamsenga, Kijiji cha Katobo, Kata ya Mpandandogo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.