Kamati ya fedha, uongozi na mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika imefanya ziara ya siku tatu kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo. Ziara hiyo imetembelea eneo la majengo ya soko la madini (yaliyopo Manispaa yam panda), eneo la ujenzi wa vibanda vya biashara (TEMESA-Ujenzi), zahanati ya Kabungu na zahanati ya Kamsanga. Miradi mingine ni ya kata ya Sibwesa, Kasekese, Mpandandogo, Katuma, Mwese na kata ya Tongwe.
Aidha, kamati hiyo imesisitiza uwazi na uwajibikaji hasa katika miradi iliyotolewa fedha na serikali (hela za UVIKO-19). Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika imepata fedha za kujenga vyumba vya madarasa ya shule shikizi 127 (vituo 24) na vyumba vya madarasa ya sekondari 69 (shule 16). Kila darasa imetengewa shilingi 20,000. Fedha hizo tayari zimeshaingizwa kwenye akaunti husika.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.