Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ufunguzi wa Bunge la 13.




Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais amewasisitiza vijana kutunza amani ya nchi na kutambua thamani yake:
“Kwa vijana, nchi hii imejengwa kwenye misingi ya kisasa. Sisi wazazi wenu tungeshawishika kufanya mlicho kifanya sasa, nchi isingekuwa na neema mnayoiona leo. Niwasihi sana vijana wa Tanzania nchi ni yenu, msikubali hata siku moja kushawishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe.”




Aidha, Mhe. Rais ametangaza kutoa msamaha kwa baadhi ya vijana waliofanya makosa kwa kufuata mkumbo. Amezielekeza mamlaka husika kuangalia kiwango cha makosa yao na kuwafutia adhabu wale ambao walijikuta wakishiriki bila kujua madhara yake waonywe, waelimishwe, kisha waachiwe warejee kwa wazazi wao.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.