Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wamesafisa Makaburi ya Mwangaza
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli John amewaongoza wafanya kazi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kuazimisha sherehe ya miaka 53 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibari kwa kufanya usafi katika maeneo ya makaburi ya Mwanganza . Makaburi ya Mwangaza yapo katika maspaa ya Mpanda, mkoani Katavi.
Makaburi hayo hutumika kuzikwa watu mbali mbali lakini pia eneo hilo ni kubwa na limezungukwa na vichaka. Kwa sasa baada ya watumishi kulifanyia usafi, wakazi wa maeneo hayo wanapita bila tatizo na kwa kujiamini.
Sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar huazimishwa kila tarehe Aprili 26 ya kila mwaka. Kitaifa, sherehe hizo ziliazimishiwa Dodoma ambapo kwa mkoa wa Katavi zilifanyika kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali.
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi kwa kuongozwa na mkuu wa mkoa Meja Generali( Mstaafu) Raphael Muhuga walifanya usafi maeneo ya soko la Buzogwe, ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda walifanya usafi maeneo ya kituo cha mabasi cha Mpanda.
Wakati huo huo, ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda walifanya usafi maeneo ya Mpanda hotel.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.