Wadau wa Elimu wilayani Tanganyika wametakiwa kushirikiana na kuongeza ubunifu ili kuweza kusaidia kuongeza ubora wa elimu wilayani humo,
Rai hiyo imetolewa jana na Bi. Suzana Nussu, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Msingi - Tamisemi wakati wa ziara yake wilayani Tanganyika ya kufuatilia maendeleo ya ubroshaji wa elimu wilayani humo kupitia mradi wa Shule Bora,
Bi. Suzana amesema kuwa ni wajibu wa wadau wote wa elimu kuhakikisha elimu inakuwa bora wilayani Tanganyika ili kuwasaidia wanafunzi kuweza kufaulu masomo yao na kutimiza ndoto zao za kielimu,
Niwaombe sana walimu wenzangu, hii kazi yetu ni kazi ya wito, tujitoe tuwasaidie watoto hawa waweze kufaulu masomo yao na kutimiza ndoto zao kielimu” amesema Bi Suzana.
Katika hatua nyingine, Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Bi. Dafroza Ndalichako ameongeza kwa kusema kuwa ni lazima jamii ihakikishe inasaidia jukumu la kuhakikisha mwanafunzi anapata elimu yake bila vikwazo vyovyote kuanzia akiwa nyumbani, mtaani mpaka shuleni.
Mradi wa Shule Bora ni mradi ambao unalenga kusaidia kuboresha elimu nchini Tanzania katika kusaidia uboreshaji wa sekta hiyo ambapo kwa siku ya jana, walitembelea shule za Msingi Vikonge na Mpandandogo hapa wilayani Tanganyika.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.