Wananchi zaidi ya 3700 wa kijiji cha Busongola, Kata ya Bulamata wilayani Tanganyika wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama kufuatia kuzinduliwa kwa mradi wa maji katika kijiji hicho.
Mradi huo ambao una thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 97 umezinduliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Busongola.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkuu wa wilaya huyo amewataka wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kuwanufaisha kwa muda mrefu zaidi na kuhudumia vizazi vingine vinavyokuja,
“Niwaombe wananchi wenzangu wa Busongola, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha hizi zote ili muweze kupata maji safi na salama, hivyo ni jukumu letu kuutunza mradi ili uweze kutunufaisha kwa muda mrefu zaidi” amesema DC Buswelu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanganyika Mhe. Yassin Kiberiti ameipongeza serikali kwa kuendelea kutekeleza vyema ilani ya chama hicho ambayo imejipambanua katika kumsaidia mwananchi kupata huduma za kijamii zilizo bora na viwango vya juu,
Aidha, Diwani wa kata Bulamata Mhe. Nicas Nibengo ameishukuru serikali kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Busongola kwa kuwapelekea mradi mkubwa wa maji ambao unakwenda kumaliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji hicho,
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kumtua ndoo kichwani mwanamke kwa kuzidi kutekeleza miradi mbalimbali ya maji safi nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani wa Chama cha Mapinduzi ambayo imejipambanu kuhakikisha inampatia mtanzania huduma zilizo bora na za kisasa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.