Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mhe. Hamadi Mapengo amewapongeza wananchi wa kata ya Ilangu kwa kuwa na moyo wa kujitolea hali na mali katika shughuli za maendeleo. Hayo ameyasema Juni 9, 2018 katika eneo la ujenzi wa sekondari ya kata ya Ilangu.
“Nawapongeza wananchi wa Ilangu na Mishamo yote kwa ujumla. Mheshimiwa Diwa, niseme ukweli kuwa mimi ninapotoka mwananchi kubeba mawe au jiwe kichwani kwa maana ya kupeleka eneo la mradi, wako tayari kutoa fedha za kutafuta gari la kusogeza mawe au matofali”. Alisema Mapengo.
Wananchi wa Ilangu wana miradi ya ujenzi wa sekondari ya kata. Hadi sasa vyumba 4 vya madarasa vimefikia kwenye hatua ya lenta, wamechimba mashimo 2 ya vyoo vya wasichana na wavulana, wamejenga nyumba inayotumika kama bohari ya muda na wameshaanza msingi wa jengo la utawala. Yote hayo wameyafanya ndani ya miezi mitatu na ni michango yao wananchi pasipo fedha za serikali.
Hata hivyo wanaenda sambamba na utengenezaji wa bara bara ya kutoka Isubangala hadi Uvinza yenye ulefu wa kilometa 26.
Naye diwani wa kata hiyo mhe. Sadick Methew alimwambia mwenyekiti kuwa aendelee kuwaamini wananchi wa Ilangu kwani hata wakipewa fedha kidogo, huwa wanashukuru kwa vitendo. Wao wakipata hata asilimia 20 za mradi, wako tayari kumalizia hizo asilimia zilizobakia.
Wananchi wana ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kabanga ambayo nayo imefikia hatua nzuri. Sambamba na miradi hiyo lakini pia wamejitahidi kupunguza tatizo la vyumba vya madarasa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.