Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Amos Makalla amehitimisha ziara yake ya kikazi wilayani Tanganyika. Amefanikiwa kutembelea tarafa zote 3 na alianza kuongea na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, madiwani na wadau wa maendeleo mbali mbali wa Tanganyika.
Septemba 3, 2018 aliongea na watumishi na madiwani na Septemba 4, 2018 alifanya ziara ya kikazi Mishamo. Septemba 12, 2018 alifanya ziara ya kikazi Ikola na Septemba 14, 2018 Mkuu huyo alienda Mwese. Hute huko alikuwa nasikiliza kero za wananchi na kufanya mkutano wa hadhara.
Mkuu huyo wa mkoa amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kujitoa katika shughuli za maendeleo na mapokezi yao yalikuwa mazuri sana. Burudani mbali mbali zilioneshwa na kikubwa zaidi ni namna anavyowatetea wananchi na kuwaahidi kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.