Wananchi wa kijiji cha Lugonesi wamefurahishwa na taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ya kumilikishwa msitu wa Tongwe Magharibi. Hayo yalisemwa kwenye mkutano wa hadhara wa kijiji Juni 5, 2018. Mkutano huo uliendeshwa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanganyika Mhe. Yasini Kibiriti, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mhe. Hamadi Mapengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuri Rojas John.
Msitu wa Tongwe Magharibi unapakana na vijiji vya Lugonesi, Lwega, Kapanga na Katuma. Vijiji vingine ni Mpembe, Vikonge, Bugwe na Bulamata. Pia kuna vijiji vya Kusi, Busongola, Kabanga, Isubangala na Mgansa. Vijiji vingine ni Ruguvu, Mlimbasi na Isenga.
Msitu huo unafaida nyingi sana kwa wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Baadhi ya faidi ni pamoja na utalii ikolojia na mazao ya misitu.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.