Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, wazindua rasmi zoezi la utambuzi na utoaji wa chanjo kwa mifugo dhidi ya magonjwa zaidi ya 13. Baadhi ya magonjwa hayo ni pamoja nahoma ya mapafu, kichaa cha mbwa, sokota ya mbuzi na kondoo, mdondo, na homa yabonde la ufa ambayo huathiri mifugo kwa kiwango kikubwa. Zoezi hilo limefanyika katika Kijiji cha Itetemya,Kata ya Karema.
Zoezi hilo limezinduliwa na Afisa Tarafa mkuu wa tarafa ya karema, Bw.Keneth Pesa Mbili,ambaye amemuwakilisha Mhe. Mkuu wa Wilaya, Onesmo Busweru. Uzinduzi huu nisehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya utoaji chanjo kwa mifugo,inayotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 hadi 2029, kama ilivyozinduliwa na Mhe. Rais wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan,tarehe 16 Juni 2025.
Wafugaji wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwekaruzuku kwenye chanjo hizo, ambapo awali mfugaji alilazimika kulipia kati yashilingi 1,000 hadi 1,100 kwa kila ng’ombe, lakini sasa gharama hiyo imeshukahadi shilingi 500 tu. Hili ni punguzo kubwa lililowezekana kutokana na ruzukuya Serikali ya Awamu ya Sita, na limeleta unafuu mkubwa kwa wafugaji katika utoajiwa chanjo.
Sambamba na shughuli hiyo, Afisa Tarafa mkuu wa tarafa ya karema, Bw.Keneth Pesa Mbili ametembelea pia mradi wa ujenzi wakituo cha Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya cha Ikola, ambao uko katika hatua ya msingi. Aidha, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Itunya, Na kuwasisitiza wasimamizi pamoja na mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi huo kwani kasi yake bado hairizishi.Mradi huu wa ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 180.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.