Wananchi wa kijiji cha Kapanga wamepongeza utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Bw. Romuli Rojas John. Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa hadhara Juni 6, 2018 wakati wa mkutano wa kuwajengea uelewa wananchi wa vijiji vinavyopakana na msitu wa Tongwe Magharibi.
Tangu kuteuliwa kwa Bw. Romuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, maendeleo kwa wananchi wa kijiji cha Kapanga yameanza kuonekana hasa katika ujenzi na uboreshaji wa vyumba vya madarasa.
Kwa sasa madarasa yanajengwa, zahanati na utunzaji wa misitu ya kijiji na vyanzo vya maji. Wananchi wameelimishwa vya kutosha namna ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.