• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe ya ofisi |
Tanganyika District Council
Tanganyika District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanganyika District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasissi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu, ufuatiliaji na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Kitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • TEHAMA na Mahusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Miradi ya Elimu
    • Usafirishaji
    • Ufugaji Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Leseni za Biashara
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Matumizi Bora ya Ardhi
    • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Kitaifa
    • Video za Shughuli za Halmashauri
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Gazeti la Mpanda Leo
    • Makala Mbalimbali

Wananchi Majalila wasaidia ujenzi kituo cha Polisi.

Posted on: September 25th, 2022

WANANCHI wa Kijiji cha Majalila, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, wameungana na serikali kujenga kituo cha Polisi kwa kuchangia fedha na nguvu kazi.

Akipokea mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya Sh milioni moja, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo Mpanda Vijijini, Seleman Kakoso, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, amemuagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi kuhakikisha wanasimamia michango hiyo kusiwepo upotevu wa aina yoyote.

Buswelu ametoa shukrani kwa wananchi na wadau mbalimbali, waliojitokeza kuchangia ujenzi wa kituo hicho.

“Serikali ya wilaya pamoja na wananchi wote na nguvu ya Mbunge Kakoso, wameamua kushirikiana kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga kituo cha Polisi cha kisasa, nawashukuru sana,” alisema Buswelu.

Awali akikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Mbunge, Katibu wa Mbunge, Said Wambali amesema ofisi ya mbunge imeona iungane na wananchi pamoja na wadau kuunga juhudi za serikali kujenga kituo hicho, ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi kituo hicho, Ramadhan Nyembe amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa michango iliyotolewa na wananchi pamoja na wadau mbalimbali, haitapotea na atahakikisha inasimamiwa kikamilifu.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Majalila wamesema kukamilika kwa kituo hicho kutawasaidia kuishi kwa amani, kwa kuwa wanaamini uhalifu utadhibitiwa na itawarahisishia kufikika kwa haraka kituoni hapo, kwani kwa sasa wanafuata huduma Kijiji cha Kibo, ambapo ni umbali wa kilomita takriban 10 kutoka kijijini hapo.

Hadi sasa ujenzi upo hatua ya msingi, ambapo wananchi wamekuwa wakichangia fedha taslimu, mifuko ya saruji, nondo pamoja na nguvu kazi ikiwa ni pamoja na kuchimba msingi wa ujenzi wa kituo hicho.

Matangazo

  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI YA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA May 27, 2025
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA NAFASI ZA DEREVA II, KATIBU MAHSUSI III NA WATENDAJI WA KIJIJI III July 07, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA July 16, 2022
  • Tazama zote

Habari mpya

  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • UKUSANYAJI WA KODI WAPAA TANGANYIKA – DC: 'NDIYO NJIA PEKEE YA KULETA MAENDELEO'

    May 27, 2025
  • HALMASHAURI ZA WILAYA YA MOMBA NA MAKETE ZAKUTANA WILAYANI TANGANYIKA KUJIFUNZA BIASHARA YA KABONI.

    May 26, 2025
  • TANGANYIKA KUENDELEA KUWEKA MIKAKATI KUBORESHA SUALA LA LISHE, WAKUU WA IDARA YA ELIMU NA WAKUU WA SHULE WAPEWA MBINU KUSIMAMIA UPATIKANAJI CHAKULA MASHULENI.

    May 13, 2025
  • Tazama zote

video

MILIONI 328 KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TFS TANGANYIKA, DC BUSWELU ASISITIZA UBORA WA MAJENGO.
Video nyingine

Mawasiliano ya Haraka

  • Taarifa kwa Umma
  • Orodha ya Madiwani
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA TANGANYIKA
  • Gazeti la Mpanda Leo
  • Habari Mpya
  • Mwanzo
  • Matukio
  • Matangazo

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikuli
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi Tanzania
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free visitor counters

Dira ya Ramani

Wasiliana Nasi

    TONGWE - MAJALILA

    Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA

    Telephone: +255-252955264

    Simu ya mkononi: 0754870344

    Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Test

Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.