Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando amekabidhi matrekta 2 kwa wakulima wa Tanganyika. Matrekta hayo aina ya John Dia yametolewa na kampuni ya PASS inayojishughulisha kwa kutoa mikopo kwa wakulima ili waweze kuzalisha kwa wingi. Mkopo wa matrekta kwa wakulima umetolewa kwa kupitia benki ya NMB na watakuwa wanarejesha kidogo kidogo.
Wakulima walionufaika na mkopo huo ni Philimon Mollo na Deo Maboti. Matrekta hayo yamekabidhiwa Desemba 11, 2018 katika viwanja vya NMB Mpanda.
Aidha, Mhando ametoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Tanganyika kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika sekta ya kilimo. Wilaya ya Tanganyika ina rutuba nzuri inayofaa kwa mazao mbali mbali. Kwa mtu ambaye akiamua kuwekeza katika kilimo biashara anaweza kuwa tajiri na watu wakashangaa.
Mazao ya kimkakati kama vile pamba, korosho, alzeti na kahawa ndiyo habari ya Tanganyika na Tanzania kwa ujumla. Watu wa kutoka sehemu mbali mbali wanaendelea kuchangamkia fursa hiyo ya kilimo kwani wilaya ya Tanganyika bado ina maeneo makubwa ya kuwekeza katika kilimo.
Eneo la uwekezaji la Luhafwe, lenye ukubwa wa hekta 46,000 limetenga ekari 27,500 kwa ajili ya kilimo uwekezaji na eneo hilo bado lipo.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.