Wahudumu afya jamii wafundwa.
Jumla ya watu saba ambao ni viongozi na wakufunzi wa watu watu 45 wa kutoa huduma ya afya ya jamii katika halmashauri za wilaya za Mpanda na Nsimbo wamejengewa uwezo wa kuwahudumia wananchi. Wananchi walengwa ni wa vijiji vya Majalila, Ngomalusambo, Vikonge na Bugwe. Vijiji vingine ni Katambike, Kasisi na Mnyamasi.
Mafunzo haya yameandaliwa rasmi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa uongozi wahudumu wa afya ya uzazi ngazi ya jamii. Wahudumu hawa ni miongoni mwa wale waliopata mafunzo na kuchaguliwa. Hawa walionekana kuwa na uwezo mkubwa zaidi ili waweze kuwasaidia wenzao huko vijijini katika kuboresha huduma hii.
Mafunzo hayo yameandaliwa na taasisi ya Jane Goodall kwa lengo la kuokoa mazingira. Mpango huu utasaidia wananchi kujitambua na kukaa pamoja kupanga idadi yaw a watoto na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo kwa uwiano wa watu.
Idadi ya waliohudhuria mafunzo haya ni 7 kutoka vijiji husika 7. Kila Kijiji ametoka 1.
Kuwawezesha kupata huduma hii kwa ukaribu zaidi, kupitia hawa wahudumu wa afya ya uzazi kwa wananchi waliokaribu na wahudumu hawa na kwa wakati wowote wakiwa na uhitaji.
Mafunzo haya ni ya muda wa siku 4.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.