Vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wamejitokeza kwa wingi katika kongamano maalum kwa vijana lenye lengo la kutoa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa mnamo Septemba 23, 2025.
Wakati wa kongamano hilo ambalo limefanyika katika Shule ya Sekondari Kabungu, vijana wameomba elimu zaidi ya masuala ya ukombozi wa kifikra na kiuchumi kuendelea kutolewa ili kuwainua zaidi katika msingi wa maisha bora.
Aidha, vijana hao wametakiwa kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, masuala ya Rushwa, tahadhari dhidi ya UKIMWI, Malaria, masuala ya Lishe bora, ushiriki kikamilifu katika michezo na kulinda utamaduni.
Sambamba na masuala hayo, lakini pia wameombwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Septemba 23, 2025 ambapo miradi mbalimbali ya kimaendeleo itatembelewa na kuzinduliwa.
Watoa mada ambao wameshiriki katika kongamano hilo ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw Oscar Mkende, Remigius Bukhay Afisa Utamaduni, Ramadhan Rashid- Dawati la Msaada wa Kisheria, Afisa Mtendaji wa Kijiji Kabungu Ziada Mnayahe, Afisa Maendeleo ya Jamii Weston Ndumbalu pamoja na Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Anisa Kitera.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.