MIRADI YA 48 BIL YATEMBELEWA WILAYANI TANGANYIKA
Kamati ya siasa ya Mkoa wa Katavi imetembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika.
Ziara hiyo imefanyika Februari 2, 2021 na imeongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Katavi, Mhe. Beda Katani. Kamati hiyo imetembelea na kujionea ujenzi wa mradi wa Bandari ya Karema katika tarafa ya Karema.
Ujenzi wa Bandari ya Karema kwa awamu ya kwanza utagharimu 47.9 Bilioni ambapo hadi sasa kazi imefikia asilimia 23. Kamati imepongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuanzisha mradi huu wa kimkakatia ambao utafungua lango la biashara za kimataifa, hasa nchi za Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Zambia nk.
Aidha, kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mnyagala na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Bw. Romuli Rojas John.
“Hongera sana Mkurugenzi wa Tanganyika. Umesimamia mradi huu vizuri kabisa na Tanganyika ndiyo Halmashauri inayofanya vizuri kwa usimamizi wa mambo mengi. Tulishitushwa na taarifa ya vyombo vya habari baada ya kusikia mmetumia 16 Milioni kwa kujilipa posho. Tumefurahi kwa kurudisha hizo fedha ili zikamilishe miundombinu mingine na tumetembelea ‘store’ na kukuta vifaa vyote vya kukamilisha ujenzi vipo”. Mhe. Katani
Kata ya Mnyagala ilipokea 200 Milioni kutoka serikali Kuu kwa ajili ya kujenga jengo la wagonjwa wan je (OPD). Ujenzi umefikia hatua ya umaliziaji.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.