Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe.Onesmo Buswelu amefanya ziara katika ukanda wa Karema, ambapo ametembelea Bandari ya Karema na kujionea hali ya ujenzi wa meli nne (4) za mizigo ulipofikia.
Katika ziara yake iliyoambatana na Kamati ua Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo unaotumia wataalamu kutoka China na wafanyakazi wa ndani walionufaika kwa kupata ajira kutokana na ujenzi wa meli hiyo.
Sambamba na hilo Mhe Mkuu wa Wilaya aliweza kushuhudia upakiaji wa madini aina ya makaa ya mawe yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi, ikiwa ni mara ya pili kwa Bandari hiyo kusafirisha makaa ya mawe.
Akizungumza kwa niaba ya Meneja mradi wa ujenzi wa meli hizo, Mohammed Chande ambaye ni Afisa Utumishi, amesema kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira kwa watu 30 ambao wanafanyakazi na kupata ujuzi mpya.
Nae wakala wa usafurishaji kampuni ya Over Seas Idrisa Asajile ameishukuru Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kufanikisha ujenzi wa bandari hiyo, ambayo imekuwa na msaada mkubwa sana katika kuongeza kipato na chanzo cha ajira kwa wananchi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.