Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imeendelea kupokea wageni kwa ajili ya kujifunza biashara ya Carbon (hewa ya ukaa) ambapo timu ya watu takribani 70 kutoka Mkoa wa Mtwara imewasili jana kujifunza biashara hiyo.
Timu hiyo iliyoongozwa na Mwanahamis Mnkunda, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili na kupokelewa na wenyeji wao ilipata fursa ya kuketishwa darasa na kupata fursa ya kuelezwa namna mradi wa carbon unatekelezwa ndani ya Halmashauri ya Tanganyika.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.