TIMU YA MADAKTARI BINGWA YAGAWA ZAWADI KWA WATOTO YATIMA.
Posted on: April 12th, 2024
Timu ya Madaktari Bingwa kutoka nchini Marekani waliofika wilayani Tanganyika hapa mkoani Katavi kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji kwa wenye changamoto mbalimbali imehitimisha awamu ya kwanza ya huduma hiyo hii leo katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika,
Timu hiyo inayoongozwa na Daktari Bingwa, Prof. Eddie Y. Chan imehimitisha zoezi hilo kwa kufurahia na kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima kutoka shule mbalimbali wilayani humo,
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa ni pamoja na vifaa vya kujifunzia kama madaftari, kalamu, peni, writing boards, midoli, peremende, nguo, mipira, na vingine vingi,
Madaktari Bingwa hao wanatarajia kurejea tena nchini mapema mwezi ujao kwa ajili ya awamu ya pili ya kutoa huduma hizo pasipo na malipo yoyote,
Hivyo basi, Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika inatoa rai kwa wale wote waliokosa kupata huduma katika awamu ya kwanza kuweza kujitokeza tena mwezi ujao ili waweze kupatiwa matibabu ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.