Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imepokea wasilisho la ripoti ya usanifu wa awali pamoja na michoro ya miradi mikubwa mitatu ya uwekezaji kiuchumi inayotarajiwa kuanzishwa.
Akizungumza mara baada ya kusikiliza wasilisho na kupokea ripoti, Mkurugenzi Mtendajii wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw Shabani J. Juma amesema kwamba, Halmashauri imedhamiria kwa dhari kuwekeza katika miradi hiyo yenye tija na kuongeza kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika hakuna kitakachoshindikana kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha, fursa za mikopo, nia madhubuti ya uwekazaji huo pamoja na malengo ya kuibua vyanzo vya mapato vilitakavyodumu muda mrefu.

Kikao hicho kilichofanyika Novemba 24, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri, kimehudhuriwa na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri(CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Shabani J. Juma, wadau mbalimbali wa uwekezaji, taasisi binafsi na za umma, Mabenki, pamoja na wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Vilevile kikao hicho kimehudhuriwa na wakala wa majengo Tanzania (TBA), TAKUKURU wilaya ya Tanganyika, TFS, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katavi, VETA Mpanda pamoja na wadau wengine wa maendeleo.


Katika kikao hicho kampuni ya Malk Architecture & Cost Ltd imewasilisha michoro ya usanifu wa awali ya miradi mikubwa mitatu. Miradi hiyo ni Jengo la kisasa la biashara (BUSINESS COMPLEX), na Masoko ya Mazao Mawili (CROP MARKETS) Katika Kijiji cha Kasekese na Kapanga.
Baadhi ya wadau waalikwa wakiongozwa na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Ndg Kichere Mwita wamepongeza juhudi za Mkurugenzi na Halmashauri kwa ujumla kwa kuanzisha mchakato huo, wakiutaja kuwa moja ya mafanikio makubwa kwa Serikali mara utakapokamilika na kuanza kutoa huduma.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.