Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewashauri wakulima wa pamba na wataalam wa zao hilo kuhakikisha wanasimamia vyema utunzaji wa Shamba darasa la pamba linalotumia mbolea ya White Diamond kama majaribio ili kuweza kupima ufanisi wake
Akihutubia wananchi waliojitokeza katika ukaguzi wa shamba darasa hilo Buswelu amesema kuwa ni vyema wakasimamia vizuri ili kuweza kujitengemezea kipato na kulia kiuchumi kupitia zao hilo
"Niwashauri kusimamia vizuri shamba darasa hili kwani mkizingatia maelekezo ya wataalamu mtajipatia mazao ya kutosha hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi"
Katika hatua nyingine Afisa Kilimo ambae pia anakahimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Philemon Mwita amesema kuwa pamba hiyo iliyopandwa 15/02/2024 imeonyesha matokeo mazuri ndani ya muda mchache.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.