Pichani:Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.
Serikali imeridhia kuachia maeneo yenye migogoro ya mipaka baina ya hifadhi za mapori ya akiba na wananchi.
Kutokana na malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi kuhusu muingiliano wa mipaka baina ya mapori ya akiba na wananchi serikali imeagiza mapori hayo yapitiwe upya na kuandaa taarifa ya kuondoa maeneo ya mamlaka za serikali za mitaa vikiwemo vijiji vilivyo ndani ya mapori hayo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja wakati akitoa tamko la serikali mkoani Katavi kuhusu migogoro inayoendelea baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi.
Mary amesema malalamiko hayo yaliibuka baada ya serikali kuyapandisha hadhi mapori matano ambayo ni pori la Luganzo Tongwe, Inyonga,Wembere Ugalla na Igombe yaliyopo mikoa ya Katavi,Kigoma na Tabora nakua mapori ya akiba Juni,2021.
Naibu Waziri Mary amesema baada ya changamoto hizo kutokea Wizara ya Maliasili na Utalii iliunda kamati maalumu ya wataalamu kutoka ofisi ya Rais ikulu,ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori (TAWA )Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wizara ya Ardhi na Wilaya ya Tanganyika ili kubaini hali halisi ya changamoto hizo na serikali ifanye maamuzi.
Aidha amesema kamati hiyo imekamilisha kazi yake na ilibaina kuwa moja ya changamoto hizo kutokea ni kutoshirikishwa kwa wadau katika mchakato mzima wa kubadilisha hadhi ya hifadhi za misitu nakuwa mapori ya akiba na pili nikuathirika kwa mapato yatokanayo na mazao ya misitu.
Hatahivyo Naibu Waziri Mary amesema pamoja nakua serikali imeridhia kuachia maeneo ya hifadhi ametoa rai kwa wananchi hao kuyaheshimu na kuyalinda maeneo yatakayo ainishwa kwaajili ya hifadhi.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu kwa niaba ya watumishi ameahidi kushirikian na Mamlaka husika kutekeleza maagizo yaliyotolewa kuhusu vijiji na maeneo mengine yaliyoingizwa ndani ya mapori hayo.
Nae Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijiji Suleiman Kakoso ameishukuru serikali kwa kuwasikiliza wananchi huku ikiiomba serikali kuendelea kutatua mgogoro uliopo katika hifadhi ya msitu wa Mpanda North.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.