Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika amefungua mafunzo ya Uwekezaji wa Hati Fungani kwenye miradi ya Kimkakati kutoka Benki ya CRDB, na UTT AMIS, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, ambao walifika Wilayani humu kufanya mafunzo haya yenye tija kwenye uwekezaji haswa kwenye mchakato wa “SAMIA INFRASTRUCTURE BOND”
Katika mafunzo hayo Mhe DC Buswelu amesema kuwa baada ya mafunzo hayo watumishi na wataalam wengine wakawe mabalozi wazuri, na kujikita zaidi kwenye kutekeleza mipango ya maendeleo.
“Tunakwenda kufungua mafunzo ambayo utekelezaji wake unakwenda kuanza kufanyika haraka, mafunzo haya ni bahati ya kipekee kwetu ikiwa sisi ni watu wa kwanza kupata mafunzo hivyo tukitoka hapa tuende kuwa mabolozi wazuri” DC Buswelu.
“Suala la Elimu ya Biashara ya Kaboni linahitaji uelewa mpana na elimu kwa watu wote kwa sababu jambo hili limebeba maslahi mapana kwa jamii nufaika na serikali, miradi itakayokubalika ikatekelezwe iwe yenye mashiko kwa sasa na kizazi za baadae” DC Buswelu.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa H/W ya Tanganyika Shaban Juma ametaja maeneo waliyojipanga kufanya uwekezaji huo, ikiwemo sekta ya kilimo, uuzaji wa viwanja (Real Estate), uwekezaji kwenye majengo ya kibiashara ikiwemo Hoteli za kisasa nk.
“Hakuna sababu ya sisi ambao tumekaa hapa Tanganyika na degree zetu na Matsers halafu siku tunaondoka hatujaacha alama yeyote, hii haifai inatakiwa tuwe na mawazo chanya yatakayoacha alama” Shaban Juma. DED H/W ya Tanganyika.
“H/W ya Tanganyika ndio Halmashauri mama na kubwa kuliko zote Mkoa wa Katavi, hivyo Halmashauri hii ina vyanzo vingi vya mapato, na tumeamua kuwezesha mafunzo haya ili kuongeza wigo mpana wa kuwekeza na kujitegemea.
“Maeneo ambayo Halmashauri imepanga kuwekeza ni Sekta ya Kilimo ambapo uwekezaji mkubwa umefanyika ikiwemo wawekazaji wakubwa katika kilimo cha Mbegu ambao ni Seedland Ltd, Meru Agro na ASA wameanza kuwekeza na wataleta Teknolojia ya Kimapinduzi kwenye Kilimo” Shaban Juma- DED H/W Tanganyika.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mhe Hamad Mapengo amewahasa viongozi wapya wa Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa ushirikiano na Madiwani pamoja na wataalam wengine, ili kutekeleza ahadi zao pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Katika Mafunzo hayo faida za kuwekeza UTT AMIS zilitajwa ikiwa ni Utalaamu, urahisi, usalama wa fedha ukisimamiwa na Mamlaka ya Masomo ya Hisa na Dhamana, Benki Kuu, CRDB, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali nk pia uwazi, ukwasi, kikomo cha uwekezaji na uratibu mzuri, ambapo mtu mmoja au kikundi chochote kinaweza kuwekeza na kupata faida baada ya muda fulani.
Nae Meneja Mahusiano Biashara na Serikal wa CRDB kanda ya Kusini ametoa ufafanuzi mzuri wa SAMIA INFRASTRUCTURE BOND.
“Benki ya CRDB ina uzoefu mkubwa wa kusimamia miradi ya Serikali, hivyo tunaangalia Serikali inataka nini na tunajivunia kwenda sambamba na matakwa ya Serikali ikiwemo kusimamia SAMIA INFRASTRUCTURE BOND ambao ni uwezeshaji ambapo Mwananchi anaweka kwenye akaunti kisha unapata faida ya 12% kwa mwaka na kwa muda wa miaka 5 unapata hela yako na faida kwa pamoja”
“Lengo la wazo hili ni fedha hizi zinazopatikana zitumike kwenye uendelezaji wa Barabara za Mitaa na Vijijini zilizo chini ya TARURA. Na nina uhakika barabara hizo zitakuwa kwenye ubora mkubwa.”
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.