Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuwatembelea waathirika wa Mafuriko katika vijiji vya Ikola na Karema vilivyopo kandokando ya ziwa Tanganyika, wilayani Tanganyika mkoani humo,RC
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mrindoko amewasilisha pole kwa waathirika wa mafuriko kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan sambamba na pole kutoka kwa serikali ya Mkoa wa Katavi,
Mheshimiwa Mrindoko amewahakikishia wakazi wa maeneo ya Karema na Ikola kuwa serikali inatambua changamoto waliyonayo na kuwataka kuwa watulivu kwani watatuma timu ya wataalamu ili wafanye utafiti kuweza kubaini kama eneo hilo bado ni salama kwa wananchi kuishi au wahamie sehemu nyingine,
Vilevile, Mheshimiwa Mrindoko alikabidhi misaada ya vyandarua, dawa za kutibu maji ili kuepukana na magonjwa ya milipuko, unga na maharage ili viweze kusaidia kaya zilizoathirika zaidi ya 200.
Mwisho, Mheshimiwa Mrindoko ameipongeza serikali ya wilaya ya Tanganyika na serikali ya kata ya Karema kwa kuitika mapema na kwenda kuwasaidia waathirika wa mafuriko kwa kuwapatia misaada mbalimbali ya chakula na malazi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.