Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Mbeya Mhe Beno Malisa leo amezindua rasmi maonesho ya Nane Nane akiwamuwakilisha Mgeni rasmi Mhe Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Ikiwa ni siku ya pili ya maonesho haya, Mhe Malisa ametaja maagizo matano ya Serikali ikiwa ni sehemu ya kuboresha sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Maagizo hayo ni kusimamia matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji, pia kuzingatia usalama wa chakula kwa kila kaya, tatu ni matumizi sahihi ya viwatilifu na kemikali za kilimo na ufugaji.
Halmashauri kuanzisha Benki ya ardhi ili kuondoa changamoto za uwekezaji wa kilimo kwa vijana, na agizo la mwisho ni kusimamia wakulima kuacha kuvuna mazao yao kabla ya muda muafaka kufika.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwemo wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa maeneo mbalimbali ikiwemo wa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika lipo katika viwanja vya John Mwakangale ambapo Maonesho haya yanafanyika, katika banda letu kuna wajasiriamali mbalimbali, maafisa ugavi na kilimo ambao wanatoa elimu kuhusu kilimo, ufugaji na uvuvi.
Karibu Kutembelea banda letu kwa elimu bora na maarifa mengi.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.