Mkuu wa Wilaya ya Tanganyia Mhe. Onesmo Buswelu amefanya ziara ya kutembelea kukagua miradi mbalimbali na kuzindua mradi wa maji uliopo kijiji cha Isubangala, Kata ya Ilangu.
Katika ziara yake hiyo Mhe Buswelu alifanikiwa kutembelea mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana shule ya Sekondari Bulamata, mradi wa maji Mazwe, mradi wa ujenzi jingo la OPD kijiji cha Ipwaga, Zahanati ya Bulamata, na kuzindua mradi wa maji kijiji cha Isubangala.
Akizungumza na wananchi katika maeneo ya ukanda wa Mishamo, DC Buswelu amewataka wakazi wote mishamo na Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika, kutokubaliwa kutekwa akili na vibaka ambao wanatumia mwanya wa siasa kuwadanganya na kuwapotosha wananchi kuhusu mambo yaliyofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Lakini pia amewataka kujiandaa vizuri na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais ifikapo Oktoba mwaka huu 2025.
Wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Isubangala utakaonufaisha wakazi Zaidi ya 2000, Mhe Buswelu amewataka wananchi kuulinda mradi huo, ili uzidi kuwanufaisha kwa muda mrefu.
Nao wakazi wa Isubangala, na Mazwe wamemshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia, kwa kuwaonna na kuwakumbuka kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo, kwani kabla ya kuwepo mradi huo walilazimika kwenda umbali mrefu kutafuta maji.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.