Serikali ya Tanzania imesema kuwa ina mpango wa kupeleka Meli Kubwa na ya kisasa katika Ziwa Tanganyika ili kuweza kurahisisha shughuli za usafirishaji na biashara kwa Mikoa inayozunguka ziwa hilo pamoja na nchi jirani za Congo na Burundi,
Hayo yamesemwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wananchi katika Viwanja vya Azimio vilivyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa anatambua uwepo wa Bandari ya Kisasa ya Karema katika Ziwa Tanganyika hivyo ili kuweza kuipa nguvu ni lazima ipatikane Meli ya Kisasa ambayo itarahisisha utendaji kazi wa Bandari hiyo,
Aidha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kusema kuwa, Serikali inajenga barabara ya Kagwira - Karema kwa kiwango cha Lami ili kuweza kuiunganisha Bandari ya Karema na Mtandao wa Barabara za Lami nchini na kuweza kuifungua kiuchumi bandari hiyo ambayo itakua kichocheo kikubwa cha uchumi kwa Wilaya ya Tanganyika na Mkoa wa Katavi kwa Ujumla,
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko Mkoani Katavi kwa Ziara ya Kikazi ya siku 3 ambapo akiwa Mkoani hapa ametembelea miradi mbalimbali ya kiuchumi na leo amehitimisha kilele cha Wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo sherehe hizo kitaifa zimefanyika Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi.
Picha na
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.