Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF )mkoani Katavi Bw. Paul Mbijima leo ametoa Semina kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kuhusiana na manufaa ya Mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo,
Bwana Mbijima amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kuendelea kuchangia mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo ya kifo, ajali, kuacha/kufutwa kazi, kustaafu na mengine mengi pindi wanapoamua kustaafu au wanapopatwa na matatizo,
Pia amewataka watumishi wa wilaya ya Tanganyika kuendelea kufanyakazi kwa bidii bila kusahau kujiandaa na maisha baada ya utumishi wa umma.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.