Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa ( OR-TAMISEMI ), mhe. Josephat Kandege amewapongeza wananchi wa kata ya Mwese iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kuchangia nguvu katika ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya cha Mwese.
Pongezi hizo zimetolewa Julai 26, 2018 wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kujionea uhalisia wa miundombinu ya kituo hicho.
“Nawapongeza wananchi wa kata ya Mwese kwa kujitolea nguvu zenu kuunga mkono ujenzi wa kituo hiki cha afya. Nimeambiwa matofali yote mmefyatua wenyewe pamoja na kukusanya mawe. Fura yangu ni kuona majengo yote yanakamilika na fedha zitakazobakia zijenge miundombinu ya kituo hiki kadri ya uhitaji”. Alisema mhe. Kandege.
Kituo cha afya cha Mwese kimepata shilingi 500 milioni kutoka serikali Kuu kwa ajili ya kujenga wodi ya akina mama, chumba cha upasuaji, maabara, sehemu ya kuchomea taka ngumu na kukarabati nyumba sita za watumishi wa kituo hicho.
Majengo ya kituo hicho cha afya yalijengo miaka ya 1950s na yalikuwa yanatumika wakati wa wakimbizi kutoka Rwanda. Hadi sasa majengo hayo yamechakaa na mengine hayafai kuendelea kutolea huduma.
Aidha, mhe. Kandege amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John kusimamisha kwanza ujenzi wa nyumba ya mpya ya mganga badala yake aelekeze nguvu kukarabati nyumba za watumishi wa kituo hicho.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.