WANANCHI TANGANYIKA WAPOKEA MWENGE 2019 KWA KISHINDO
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019, Mzee Ali amewasifu wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika ) kwa kujitokeza na kushiri kupokea na kukimbiza Mwenge. Pongezi hizo zimetolewa Aprili 16, 2019 wakati wa makabidhiano ya Mbio za Mwenge kati ya Mkoa wa Katavi na Kigoma.
“Wananchi wa Tanganyika walijipaka haswaa na wanajua nini maana na umuhimu wa Mwenge. Wametupokea vizuri na kila tulipopita tulikuta wananchi wamejipanga jiani na kikubwa zaidi wametuandalia hadi urojo, tumejihisi tupo Zanzibar.” Alisema Ali.
Mwenge wa Uhuru umezindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea na kukagua jumla ya miradi 13 yenye thamani ya shilingi 2,987,469,044.93. Miradi yote imekubaliwa bila tatizo kwani ilikuwa kwenye viwango vinavyokubalika.
Aidha, viongozi wa wilaya ya Tanganyika walipongezwa kwa kusimamia vizuri miradi ya wananchi kwani serikali ya awamu ya tano haitaki watu wanaochezea hela za wananchi.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa wilayani Tanganyika katika viwanja vya shule ya sekondari Kabungu ukitokea Halmashauri ya wilaya ya Manispaa ya Mpanda na kukesha katika viwanja vya mpira Ifumbula ambapo umekimbizwa wilayani Tanganyika kwa jumla ya 231.4 kilometa.
Wananchi wa wilaya ya Tanganyika walikuwa na shauku ya kuupokea Mwenge, kulikuwa na vikundi vya burudani vya wananchi wenyeji zaidi ya 20, seti 3 za mziki , sinema na burudani mbali mbali. Watu hawakulala na waliburudika kuanzia mchana hadi asubuhi.
Naye mratibu wa Mwenge wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika) Bw. Sylvanus Ntiyakenye ameeleza siri ya kufanikisha sherehe za mbio za Mwenge kuwa ni kuwashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo na wanakamati kwa kuwaweka wazi hasa katika matumizi ya michango waliyochangia.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.