HAMASA UCHAGUZI OKTOBA 29.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika,Mheshimiwa Kagemlo charlse, ameongoza bonanza maalum lililowakutanisha wananchipamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika katika kuhamasishaushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29Oktoba 2025.
Bonanza hilo limefanyika katika Kata ya Karema,limelenga kuwahamasisha wananchi wa maeneo hayo na Jimbo la Tanganyika kwaujumla kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka nawanaostahili kuwaletea maendeleo.
Akizungumza katika tukio hilo, Mhe. Kagemlo amewatakawananchi kutumia haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu, na kujiepusha naaina yoyote ya vurugu kipindi chote cha uchaguzi. Amesisitiza kuwa amani ninguzo muhimu ya maendeleo, hivyo kila mwananchi anapaswa kuwa mstari wa mbelekuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya utulivu na usalama.
“Kura yako ni sauti yako. Njoo upige kura kwaamani ili kumchagua kiongozi unayemwamini atakupeleka kwenye maendeleo,”alisema Mhe. Kagemlo.
Tukio hilo limepambwa na michezo mbalimbalikama mpira wa miguu, mpira wa pete, kukimbiza kuku,kuvuta Kamba na kukibia naviroba, burudani ya muziki Pamoja na kwaya na ujumbe wa amani, likiwa ni sehemuya juhudi za Tume ya Uchaguzi na wadau wengine katika kuhakikisha wananchiwanajitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi kwa njia ya Amani.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.