WANANCHI WA VIJIJI VYA MSITU TOGWE WATABASAM
Wananchi wa vijiji vinavyozungwa na msitu wa Tongwe Magharibi wameanza kufurahia baada ya kusikia waziri wa maliasili na utalii Mhe. Hamis Kigwangalla amesaini kusudio la kumilikisha msitu huo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Msitu huo wenye ukubwa wa zaidi ya hekta 330,000 umezungukwa na vijiji 15 na elimu ya kuwaelimisha na kupokea maoni ya wananchi kwa awamu ya pili imeanza mwishoni mwa Novemba, 2018 na itaendele hadi mwanzoni mwa januari 2019.
Furaha ya wananchi ilionekana mara tu baada ya kaimu Mkuu wa idara ya ardhi na maliasili Bw. Elisha Mengele kuwaeleza kwenye mikutano ya hadhara inayoendelea katika vijiji hivyo vinavyozungukwa na msitu wa Tongwe Magharibi.
“Ndugu wananchi mnakukumbuka kuwa mwanzoni mwa mwezi wa sita timu ya viongozi wa wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na uongozi wa chama na serikali wa wilaya ya Tanganyika walifika kuwaelimisha faida za msitu wa Tongwe Magharibi kwa wananchi endapo msitu huo utamilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda”. Alifafanua Elisha Mengele.
Aidha, faida zitokanazo na msitu huo wa Tongwe Magharibi ni pamoja na chazo cha kudumu cha mito zaidi 16, ajira kwa vijana 6 kwa kila kijiji kilichozungukwa na msitu huo, uvunaji wa hewa ya ukaa na ufugaji wa nyuki. Faida zingine ni pamoja na shughuli za kiutalii kwani ndani yam situ huo kuna sokwe wa kutosha.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.