Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe Onesmo Buswelu ameitaka timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, kufanya tathmini ya miradi mipya itakayopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru ifikapo Septemba 2025.
Mhe Buswelu ameagiza hayo leo kwenye kikao cha kujadili miradi ya Mwenge, ambacho kilihudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wataalam wa Menejimenti ya Halmashauri.
“Nawaagiza baada ya kikao hiki mpitie miradi yote na mfanye tathmini ya kina kuhusu hali hali ya miradi hiyo, kabla ya Mwenge wa uhuru kufika, kwa sababu bado tunasua sua” DC Buswelu.
Lakini pia, amegusia suala la kusimamia na kuvilea vikundi vyote vinavyopokea mikopo ya mapato ya ndani ya 10% ili visiishie kufa.
“Maendeleo ya Jamii mnajukumu ya kuvilea na kuvisimamia vikundi vyote ili visife, kaeni navyo na muwaoneshe fursa zilizopo” DC Buswelu.
Kwa upande wa Mkuu wa TAKUKURU Chacha Kichere Mwita ameitahadharisha Menenjimenti kutoanzisha mchakato mpya wa utoaji wa fedha kwenye miradi hiyo ambayo itahitaji taratibu za kisheria ili ikamilike, hiyo ni kutokana na Baraza la Madiwani kuwa limevunjwa.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.