Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw Shaban Juma amekutana na Kikundi cha Wafugaji wa Ng’ombe cha BADIMI RANCH, ambacho kilikuwa na mgogoro wa Kimkataba juu ya eneo la ufugaji na malisho.
Katika kikao hicho kilichafanyika Desemba 02, 2024 ofisini kwake na kuwapa ushauri na njia za kufanya ili waweze kupata eneo la ufugaji.
“Kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa eneo la ufugaji, na hii leo tumekutana na kikundi cha wafugaji-BADIMI RANCH kuanzisha mchakato mpya wa kimkataba ambao utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili” DED Shaban Juma.
“Nimewambia warudi wakakubaliane na wenzao wachague njia mbili, tuwape eneo ili wafanye uwekezaji wao kwa sababu tayari eneo lipo, au tuwape pesa zao ambazo nazo zipo.
“Serikali imejipanga vizuri kuwahudumia wananchi wote na wawekezaji, hapa Tanganyika kuna maeneo mengi ya uwekezaji yametengwa hivyo nawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza.” Bw Shaban Juma-DED H/W ya Tanganyika.
Kwa upande wa wawakilishi wa kikundi hicho ambaye ni Mjumbe wa Kamati tendaji Chama cha Wafugaji Tanzania, kanda ya Kaskazini Dkt Christopher Nzela alisema wanepokea ushauri wa Mkurugenzi na wapo tayari kuufanyia kazi, ili waendelee na kazi yao ya ufugaji.
“Ushauri aliitupa Mkurugenzi ni mzuri sana, ametupa machaguo mawili eneo au pesa zetu kwa taarifa yake ni kwamba zote, ila hitaji letu kubwa ni eneo na tunaamini tutakuwa na mwisho mzuri hatimaye tuendelee na zoezi la ufugaji kama ambavyo lengo letu lilivyo” Dkt Nzela.
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ina maeneo mengi ya uwekezaji kwa kilimo, ufugaji nk hivyo wadau wote wa maendeleo na wawekezaji, tunawakaribisha sana kuwekeza kwetu.
Tanganyika safi na atakaye aje.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.