Wananchi wilayani Tanganyika Mkoani Katavi wameshauriwa kuweka akiba na kuwekeza fedha zao wanazozipata kutoka vyanzo mbalimbali ili ziweze kuwasaidia hapo baadae,
Ushauri huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw. Shaban Juma Juma alipokuwa akifungua mafunzo ya siku 6 kwa vikundi vinavyonufaika na Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF).
Bw. Shaban Juma ameongeza kwa kusema kuwa ni wakati sasa jamii lazima iamke na kujijengea utaratibu wa kuwekeza fedha wanazozipata kwani ndio mkombozi pekee wa maisha yao ya hapo baadae,
“Lazima jamii yetu itambue umuhimu wa uwekezaji wa fedha wanazozipata, hata sisi watumishi lazima tuweke akiba ya fedha zetu ili ziweze kutusaidia pindi maisha ya utumishi yatakapofika ukomo” amesema DED Shaban.
“Akiba zetu tuwekeze sehemu ambazo zinaweza kutupatia faida ambayo itasaidia kuendeleza maisha au mipango yetu ya kiuchumi. Unaweza kujiunga kwenye vikundi, Vikoba, au kuweka Benki” ameongeza DED Shaban,
Mafunzo hayo ambayo yatadumu kwa takribani siku sita, yanafanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika na yanakusudia kuyafikia makundi mbalimbali hususani yale yanayonufaika na Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini yaani Tasaf.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.