MKURUGENZI MPYA WA TANGANYIKA AANZA NA MAMBO MAPYA 5
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika, Bw. Shaban Juma Juma amedhamiria kuijenga upya Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa kuanza kubadilisha mfumo wa kiutendaji kwa watumishi. Mambo ambayo ameyaanzisha mapya na kuyasimamia na kuyatolea maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ni pamoja na;
Kuweka mazingira wezeshi kwa kila idara na vitengo kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Katika kuhakikisha hili linawezekana, Bw. Shaban Juma ameanzisha utaratibu wa kila mwezi kuweka mgawo wa mapato ya ndani kwa kila idara na vitengo kulingana na bajeti iliyotengwa.
Kila mtumishi kupimwa kwa kazi aliyoajiriwa nao. Watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika ni muhimu na hakuna aliye muhimu kuliko mwingine. Kila mtumishi ameajiriwa kwa kuzingatia sifa na uwezo wa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi na siyo vinginevyo kutokana na taaluma yake (mambo aliyosomea).
Ukusanyaji wa mapato, Kila mtumishi anawajibika kuhakikisha anakusanya au kusaidia upatikanaji wa mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika. Hii ni kutokana na utaratibu wa kutengeneza mfumo wa kila mtumishi kuwa mnufaika wa makusanyo ya mapoto kwa njia moja au nyingine.
Kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha. Miradi ya umma itatekelezwa kwa uwazi na ushirikishwaji wa jamii hatua kwa hatua. Hii itaimarisha uaminifu na kujitolea kwa jamii kuchangia shughuli za maendeleo za jamii.
Kuimarisha upendo kati ya watumishi kwa watumishi. Hii itaongeza ufanisi wa kiutendaji na kupunguza malalamiko na manunguniko kwa watumishi. Hili limeanza kuzaa matunda kwani watumishi wengi wameanza kupata nguvu za kuchapa kazi tena hata kwa muda wa ziada.
TONGWE - MAJALILA
Sanduku la barua: S.L.P 01 KATAVI - TANGANYIKA
Telephone: +255-252955264
Simu ya mkononi: 0754870344
Barua pepe: ded@tanganyikadc.go.tz
Copyright ©2018 Tanganyika-DC . All rights reserved.